Mama mmoja alitambulika
kwa jina la Verphy Kudi anadaiwa kumuacha ndani mtoto wake wa kike mwenye umri
wa mwaka mmoja na miezi 8 kwa siku sita na kupelekea kufa kwa njaa.
Msichana huyo anadaiwa
aliondoka nyumbani kwake na kwenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya
kutimiza miaka 18 ambapo alimuwacha mtoto ndani na yeyekuondoka.
Uchunguzi wa Daktari
ulionesha kwamba kifo cha mtoto huyo kilisababishwa na njaa, upungufu wa maji
mwilini na homa.
Mahakama ya Lewes Crown
iliyopo England Uingereza imemuhukumu mama huyo kifungo cha miaka tisa gerezani
baada ya kukiri kutenda kosa hilo.