ALI KIBA APATA TUNZO MBILI KUTOKA YOUTUBEStar wa muziki nchini  Tanzania  Ali Kiba amepokea tunzo 2  kwa pamoja (Gold & Silver) kutoka kwenye mtandao wa Youtube.

Msanii huyo  amefanikiwa kupata tuzo ya gold baada ya Kufikisha zaidi ya wafuasi (Subcribers) Milioni 1 Katika channel yake ya Youtube hivi karibuni.

Ali Kiba pia amepata tuzo ya Silver ikiwa ni baada ya Channel yake ya KingsMusicRecords Kufikisha Subcribers laki tano.