ANNA MAKINDA AWANYOSHEA KIDOLE WANAOHUSISHA SENSA NA CHANJO YA COVID 19Spika msaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ni Kamisaa wa Sensa ya watu na maakaazi, Anna Makinda  amewataka watu kuondoa  imani potofu kuwa zoezi la Uhesabu Watu na Makazi linahusiana na Chanjo ya COVID19 na kusema kuwa jambo ambalo si kweli.

 Kamisaa Anna amesema kuwa vijana waliohitimu Vyuo Vikuu wanaojitolea maeneo mbalimbali watapewa kipaumbele katika kupewa ajira za kuhesabu watu.

 Zoezi la kutoa elimu kuhusu Sensa ya watu na makaazi itakayofanyika 2022 inaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbli nchi nzima.