Wajumbe wa kamati sensa wilaya ya magharibi B wametakiwa kuhakikisha wanatoa hamasa kwa wananchi ili waweze kushiriki Katika sensa ya watu na makazi wakati itakapofika na kupata takwimu halisi zitakazoiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya magharibi B hamida mussa khamis wakati alipokuwa akizinduwa kamati ya sensa ya wilaya magharibi B huko katika ukumbi wa baraza la manispaa wilaya ya magharibi B.
Mh Hamida ambae pia Ni mwenyekiti wa kamati ya sensa ya watu na makaazi katika wilaya hiyo amesema ili serikali iweze kufanikiwa katika sensa ya Watu na makaazi mwaka 2022 hakuna budi kwa kamati hiyo kutekeleza majukumu ipasavyo ili kutekeleza matakwa ya serikali.
Aidha amesema sensa ya mwaka huu ni tofauti na zilizopita kwani itatoa idadi halisi ya Wananchi katika ngazi ya shehia na kuainisha Mambo mbalili mbalimbali ikiwemo idadi ya wafanyakazi,vifo vinavyotokana na marafhi, vizazi na wanaojuwa kusoma.
Mapema akitoa maelezo katibu wa kamati ya sensa katika wilaya ya magharibi B Haji Ame Haji amewataka wajumbe hao kusimamia uhaulishaji wa mipaka katika shehia,usambazaji wa vifaa vinavyohusiana na sensa, kuelimisha,kuhamasisha na kuhakikisha watu wanahesabiwa Mara moja katika maeneo yao.
Nao wajumbe wa kamati ya sensa ya Watu na makaazi katika pwilaya ya magharibi B wameahidi utekeleza majikumu yao Kama inavyotakiwa ikiwa ni kusimamia na kutekeleza miongozo ya sensa ya Watu na makaazi mwaka 2022 kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
Story na Takdir Ali.