KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII BARAZA LA MANISPAA MAGHARIB B LAPANIA KUTATUA CHANGAMOTO MASKULINIKamati ya huduma za jamii Baraza la manispaa wilaya ya magharibi B imeahidi kushirikiana na serikali kuu katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo yaliopo katika skuli za serikali na binafsi.


Akizungumza katika ziara ya kukaguwa usafi skuli ya chukwani, Kijitoupele na Kombeni mwenyekiti wa kamati hiyo katika Baraza la manispaa wilaya ya magharibi B thuwaiba jeni Pandu amesema baadhi ya skuli zinakabiliwa na tatizo la wafanya biashara kutozingatia maagizo ya wataalamu wa afya na uchafu wa vyoo, Mambo ambayo yanakwamisha maendeleo ya skuli hizo.

Amesema lengo la ziara hiyo Ni kutoa elimu kwa Wafanyabiashara wa maeneo ya skuli ili wafahamu njia za kujikinga na matatizo yanayoweza kujitokeza.

Aidha amesema jukumu la kusomesha Ni la watu wote hivyo amewaomba wazazi na walezi kushirikiana na waalimu ili kufanikisha utoaji wa elimu kwa watoto wao.

Nao waalimu wakuu wa skuli hizo wamesema wanajitahidi kutoa elimu kwa Wafanyabiashara katika maeneo ya skuli Kama vile wauza urojo,baadia na juisi lakini baadhi yao wanakaidi na kuhatarisha afya za wanafunzi.

Hata hivyo wameahidi kusimamia maagizo waliotolewa na kamati hiyo ili kuwakinga athari zinazoweza kuwapata watoto wao ikiwemo kipindupindu na  matumbo ya kuharisha.