KISA CHA MWANAMAMA ALIEJIFUNGUA KIUMBE CHA AJABUAmakwahakika kuishi kwingi ndio kuona mengi katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja  alitambulika kwa jina la Regina Mataba anekisiwa kuwa na umria  wa miaka 46 mkazi wa Sima Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu amedai kujifungua mnyama aitwae Kalunguyeye  jambo ambalo limewashangaza wengi.


Mwanadada huyo ambae amejifungua wakati ujauzito wake ukiwa na miezi minne ambapo amesema  mnamo Septemba 12, 2021 alihisi uchungu na kwenda chooni ambako alijifungua mnyama huyo ambae awali alionekana kama panya buku ila alimwagiwa maji ya baraka na ikagundulika kuwa ni mnyama aina ya Kalunguyeye na alikufa baada ya siku mbili.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bariadi Dk. Costantine Emmanuel amesema kwenye vipimo vyote vilivyofanyika vimeonesha Mama huyo hakuwa na ujauzito ambapo pia mji wa mimba haukuonesha kama katoka kujifungua hivi karibuni, kwa upande mwingine mmoja wa Viongozi wa dini kutoka Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Luka Katekista Ibrahimu Gibayu aliongoza ibada fupi ya kukiteketeza kwa moto kiumbe hicho.