POLISI ALIYE ALIYEMUUWA FLOYD AKATA RUFAA BAADA YA KUHUKUMIWA MIAKA 22

 Aliyekua Polisi  wa Minnesota  ncjni Marekani Derek Chauvin amabe amehukumiwa kifungo cha miaka 22 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua George Floyd May, 25 2020, amekata rufaa.

Derek ambaye anatajwa kuwa Polisi wa kwanza Mzungu kuwajibishwa kwa mauaji ya Mtu mweusi Minnesota, amekata rufaa hiyo katika Mahakama ya Rufaa Minnesota akipinga hukumu hiyo na kusema alionewa na hakupewa haki zake za msingi wakati wa maamuzi.