SMZ KUWACHUKULIA HATUA WAFANYABIASHARA WANAOPANDISHA BEI ZA BIDHAA KIHOLELA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali hatosita kumchukulia hatua mfanyabiashara yoyote atakaebanika kupandisha bei za bidha bila ya kufuata taratibu kutoka taasisi husika kwa masla binafsi.

Mhe. Hemed alileza hayo wakati akitoa hotuba ya kuaghirisha Mkutano wa Nne wa baraza la Kumi la wawakilisha katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Chukwani jijini Zanzibar.

Alisema, mbali na sababu ya kupanda bei ya bidhaa katika soko la dunia lakini kumekuwepo na vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu wanaosababisha kupanda kwa bei za bidhaa kunakosababishwa na kuzingatia masalahi yao binafsi na kuacha kuwaangalia wananchi wanyonge.

Aliwataka wafanyabiasha kuachana na visingizio visivokuwa na msingi vinavyopelekea kupandisha bei kiholela bila ya kupata maelekeo kutoka Wizara ya Biashara na maendeleo ya Viwanda.

Mhe. Hemed aliendelea kuuwagiza Uongozi wa Shirika la Bandari pamoja na taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria dhidi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu na wanaoingiza bidhaa zilizo chini ya kiwango.

Aidha, Mhe. Hemed alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali wasiokuwa waaminifu wanaoshiriki katika vitendo viovu ikiwemo utoaji wa nyaraka, leseni na vyeti mbali mbali kwa kupatiwa watu wasiostahiki kwa kutumia njia ya rushwa.

“Mhe. Spika Vitendo hivi vinaitia aibu serikali na kusababisha lawama kwa wananchi wake” Alieleza Mhe. Hemed

Katika kuipatia Ufumbuzi kadhia hiyo Makamu wa Pili aliwaagiza na kuwakumbusha viongozi wenye dhamana kuacha mara moja kujihusisha na jambo hilo na badala yake wajitahidi kuwasimamia watendaji walio chini ya dhamana zao ili kuwaondelea wananchi usumbufu na kuhakikisha wananchi wote wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Akizungumzia suala la miundombinu ya bara bara Makamu wa Pili wa Rais alisema serikali ilipanga kujenga Jumla ya kilomita Mia mbili na Ishirni (220) za bara bara za ndani kwa kiwango cha lami lakini kutokana na umuhimu uliopo serikali imeamua kujenga Kilomita Mia mbili na Sabiini na tano (275).

“Pia serikali itajenga kilomita Mia mbili na Ishirini na Moja (221) za bara bara kuu ambapo kwa kipindi hiki tayari ujenzi wa barabara ya Wete Chake umeanza kwa hatua za awali” Alisema Makamu wa Pili wa Rais

Akiendelea na houtuba yake, Mhe. Hemed alitumia fursa hiyo kuwakumbusha mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya kufanya ziara na kuskiliza kero na malalmiko ya wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi inayoendelea kushika hatamu kila uchao.

Alieleza kuwa, ni jambo linalosikitisha kuona changamoto ndogo ndogo za wananchi zinasubiri kutatuliwa na viongozi wakuu wakati viongozi walipo katika ngazi mbali mbali wana jukumu la kushugulikia changamoto hizo katika ngazi walizokuwepo.

Akigusia juu ya suala la kilimo Makamu wa Pili wa Rais aliiagiza Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kukamilisha miradi waliyoianza na kuhakikisha Zanzibar inajitosheleza kwa chakula kupitia sera na mikakti iliyopo.

Kuhu zao la karafuu alifafanua kwamba serikali shirika la ZSTC wanaendelea na zoezi la kununua karafuu ambapo hadi sasa nusu ya makadirio ya ununuzi wa karafuu zimeshanunuliwa.

Vile Vile Makamu wa Pili wa Rais ameonesha kusikitishwa kwake kutokana na taabia inayofanywa na baadhi ya watu wanaouza karafuu katika shirika hilo la serikali kwa kuuingiza vitu visivyohitajika katika bidhaa hiyo hali inayoplekea kuzichafua karafuu kwa kuongeza vitu mbali mbali.

“Mhe. Spika nakerwa sana na changamoto iliopo ambapo baadhi ya watu wanaendelea kununua karafuu za wananchi vijijini kwa kutumia vikombe, hapa natoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na wilaya pamoja na mashesha kutoa elimu kwa wananchi kwenda kuuza karafuu zao katika shirika la ZSTC” Alieleza Mhe. Hemed.

Akizungungumzia juu ya mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) alisema mfuko huo unaendelea kuwa chahu ya kuwasaidia wananchi walio maskini katika jamii ambapo serikali zote mbili zimo katika utekelezaji wa kipindi cha pili cha mpango wa kunusuru kaya maskini.

Alieleza kuwa, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais imendelea kuratibu kwa kuwarejesha katika mfumo wa malipo kwa kaya 1,536 (Unguja 666 na Pemba 870) kutoka kaya 2,459 (Unguja 915 na Pemba 1,544) sawa na asilimia 62 za walengwa waliorejeshwa na asilimia 38 na kaya zilizobakia ambazo zinaendelea kufanyiwa uhakiki wa kina.

Akizungumzia sekta ya utalii Mhe. Hemed alieleza serikali imedhamiria kuendeleza sekta hiyo, kwa kuchukua hatua mbali mbali ikiwemo kuansha mpango maalum wa kufufua utalii (Torism Recovery Plan) mpango ambao umeanza kutoa matokeo Chanya kwa kuongezeka kwa mashirika yay a ndege ya kimataifa kutoka Uholanzi na KLM  la Ujeruman.

Kwa upande wa maradhi ya UVIKO-19 Makamu wa Pili wa Rais alieleza serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti ya kujikinga dhidi ya maradhi hayo ambapo zoezi la chanjo linaendelea kutolewa katika vituo mbali mbali vya Afya Mjini na Vijijini bila ya gharama yoyote huku akiwaomba wajumbe wa baraza hili kuwahimiza wananchi katika majimbo yao umuhimu wa chanjo hiyo kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Hemed alizungumzia suala la sensa ya watu na makaazi ambapo aliwataka viongozi na wanachi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kufanikisha zoezi hilo kutokana na gharama kubwa zinazotumika katika kuendesha zoezi hilo.

Alisema kwamba, sensa ya idadi ya watu na makazi ni jambo la msingi ambalo litasaidia kupanga vizuri mipango ya maendeleo ya wananchi kwa miaka kumi ijayo kwa kupata takwimu halisi na sahihi ya idadi ya watu na makaazi.

Katika sekta ya michezo, Mhe. Hemed alisema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi imechukuwa jitihada za kutafuta wadhamini kwa ajili ya ligi mbali mbali kwa msimu wa 2021/2022 ambapo utaanza hivi karibuni ambapo jumla ya fedha Millioni Mia Tisa na Arobaini laki Tano na Elfu Kumi za Kitanzania zimechangishwa (940,510,000/=)

Jumla ya miswada mitatu imejadiliwa na kupitishwa ikiwemo

Mswada wa sheria ya kuanzisha Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na kuweka usimamizi mzuri wa shughuli za kiislam Zanzibar

Mswada wa sheria ya marekebisho ya Sheria mbali mbali na kuweka mashrti bora ndani yake.

Mswada wa sheria ya kuanzisha Ofisi ya msajili wa Hazina na usimamizi wa mali za Umma na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Baraza limeakhirishwa mpaka siku ya Jumatano Disemba 15, 2021 saa Tatu Kamili za Asubuhi (3:00)