TANZANIA YAENDELEA KUPIGA HATUA YA KUIMARISH MAENDELEOTanzania itandelea kupiga hatua na kuimarisha ustawi na maendeleo ya wananchi wake kupitia serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suhulu Hassan.

Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa ambae pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo akiwa katika ziara maalum ya kuimarisha chama wakati akisalimiana na  wanachama na wananchi wa Shina Nambari Tano Kata ya Kibirashi Wilaya ya Kilindi.

Mhe. Hemed aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna kila sababu ya kumuunga mkono Rais Samia kwa kudumisha Amani na Utulivu kutokana na Dhamira ya dhati aliyonayo Kiongozi huyo katika kuwatumikia wananchi wake.

Alisema kuwa, serikali ya  awamu ya sita inayotekeleza Ilani ya CCM itaijenga Barabara ilioanzia Handeni kupitia Kilindi na kumalizia Songe kwa kiwango cha lami ili kurahisha mawasiliano na kuinua hali ya uchumi kwa wakaazi wa wilaya hiyo.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alitumia fursa  hiyo kuwahamasisha wananchi wa Wilaya ya Kilindi kujitokeza kwa wingi kushiriki zaoezi la sensa ya watu na makaazi  muda utakapowadia.

Alisema kushirikia katika zoezi hilo kutaisadia serikali kuweza kupanga mikakati ya maendeleo kwa  wananchi wake sambamba na kupata takwimu sahihi itakayosaidia kutatua changamoto mbali mbali zinazolikabili taifa kupitia sekta ya Afya, Elim na sekta nyengine za kijamii.

Akizungumzia suala la maradhi ya UVIKO-19 Mjumbe huyo wa kamati kuu aliwakumbusha wanachi kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ambayo inatolewa bure na serikali kwa lengo la kupambana na maradhi hayo hatarishi.

Nao Viongozi wa Jimbo hilo la Kilindi Mbunge Mhe. OMAR KIGUA na Diwani Mhe. Abubakari walisema Pamoja na mikakati mizuri iliopangwa na serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo ikiwemo kutengwa kwa Shillingi Millioni Mia Tano wamemuomba Mlezi wa Mkoa huo kutoa msukumo maalum kwa ajili ya kufanikisha  lengo hilo.

Akisoma risala Katibu wa shina Nambari Tano kata ya Kibirashi Pili Juma Magambilwa alimuomba Mjumbe huyo wa kamati kuu na Mlezi wa Mkoa wa Tanga kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanachama na wakaazi wa eneo hilo ikiwemo kupatiwa Tawi Pamoja na kuifanya Zahati yao kuwa Kituo cha Afya ili iweze kutoa huduma kwa wagonjwa.

Akiendelea na ziara yake katika Wilaya Hiyo Mhe. Hemed alifika katika Skuli ya Sekondari Mafisa na kuweka Jiwe la Msingi Bweni la wanafunzi wanaume wa kidato cha Tano na Sita.

Akilikagua Bweni hilo Makamu wa Pili wa Rais alionesha kuridhishwa kwake na matumizi ya fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi huo ambalo linawanufaisha wanafunzi wapatao Themanini (80).

Akitoa Shukrani kwa niaba ya wananfunzi wa skuli hiyo Joice Msengelwa Pius alisema wanafunzi wa skuli hiyo wanaipongeza Serikali kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo hali iliyopelekea kupatikana kwa huduma za msingi katika skuli hiyo.

Katika Kuunga Nguvu jitihada za Wazazi na wananchi wa Mafisa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alihamasisha mchango maalum kwa ajili ya kumalizia Bweni jengine la kulala wanafunzi ambalo ujenzi wake umegharamiwa na wananchi wenyewe.

Wakati wa Mchana Mjumbe huyo wa Kamati kuu alipata fursa ya kuzungumza na Viongozi wa Wilaya ya Kilindi Pamoja na wanachama kupitia Mkutano wa ndani katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.

Katika hotuba yake Mhe. Hemed aliwakumbusha viongozi hao kufuata Katiba,taratibu na kanuni za chama  kwa kuachana na tabia ya kutengeneza makundi mapema kabla ya wakati kufuatia uchaguzi wa Chama unaotarajiwa kufanyika 2022.