WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUTAFUTA WAALAMU KABLA YA KUANZISHA MIRADI

 


Afisa mipango kutoka idara ya maendeleo ya vyama vya ushirika Zanzibar Haroun Ilias Muhammed amewashauri wajasiriamali wa Vikundi vya ushirika kutafuta wataalamu kabla ya kuanzisha miradi ili kuepuka hasara inayoweza kujitokeza.Amesema baadhi ya wajasiriamali wanaanzisha miradi ya kilimo , biashara na ufugaji bila kupata ushauri wa wataalamu husika jambo ambalo linasabisha kupata hasara na kutofikia malengo waliokusudia.


Akizungumza katika mafunzo ya miezi sita kwa wajasiriamali wa vikundi vya ushirika katika Wilaya ya Kati huko skuli ya binguni amewataka kufanya tathmini ya shughuli wanazozianzisha na kuacha kufuata mkumbo.


Aidha amewataka kubadili mitazamo ya zamani kutumia ya kisasa ambayo itaweza kuwaletea tija ya kimaendeleo Katika vikundi vyao.


Kwa upande wake Afisa wa vyama vya ushirika Katika wilaya hiyo saidi khalfan amewataka wajasiriamali hao kujiunga na sacos kuu ya wilaya (boresha maisha yako sacos) ili kuweza kupata fursa zilizomo ikiwa ni pamoja mikopo ,ushauri na elimu .


Aidha amewataka kufikisha ekimu waliopatiwa kwa wenzao ili iweze kuleta tija na mabaliko kwa familia Taifa kwa ujumla.


Nao wajasiriamali wa vikundi vya ushirika Katika wilaya ya Kati wameomba kupatiwa mbolea kwa wakati, mabibi na mabwana shamba ,vitendea kazi na ufadhili wa miradi wanayoianzisha ili kuepuka hasara wanazozipata Mara kwa Mara ikiwemo kufa vipando vyo na mifugo wanayoifuga.


Hivyo wameomba kupatiwa elimu na kufanyiwa ukaguzi wa Mara kwa Mara  ili kubaini matatizo yanayowakabili na kufanyiwa kazi kwa haraka.

Story Na Takdir Ali.