Wazo bora la BiasharaWazo la Biashara ni moja ya jambo linalowaumiza watu wengi sana, na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima. Aidha kumekuwa na mafunzo mengi kupitia vitabu, semina na makongamano ya kuelimisha jinsi ya kuandaa wazo bora la biashara pamoja na kutumia nyenzo za kisiasa(tools) katika kutathmini wazo lako la biashara. 


HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO BORA LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIO NAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe ni mtaalam wa kupika na watu wanakusifia juu ya mapishi yako, kwanini usianzishe biashara yako ya kupika hususani katika Dunia ya leo ambapo watu wengi wako busy na kazi na hawana muda wa kupika?  
Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza ya pekee ya kupata wazo bora la biashara, wajasirimali wengi waliofanikiwa wanafanya biashara kutokana na ujuzi walionao kuliko kutegemea kuajiri watu wakufanyie biashara unayoianzisha.

2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA

Hobby ni moja ya maeneo ambayo unaweza kuyatumia kuweza kujitengenezea kipato, mathalani kama wewe unapenda masuala ya kujipamba na kupamba wengine unaweza kabisa kuwa 'Makeup artist' na kama wewe ni mtu wa kupamba nyumba na kufatilia masuala ya kupendezesha nyumba unaweza kuanzisha biashara ya Interior Design.


3. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njia zinazotumika kwa sasa sehemu nyingi sana Duniani, Unaweza nunua popular Brand na kuifanyia kazi, ingawa mara nyingi kuna mashariti huambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brand yenyewe, njia hii ni maarufu sana hasa katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE.

Muhimu la kuzingatia ni kuwa usitumie Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa taarifa inaweza kukuletea matatizo ikiwemo kufilisiwa.


4. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kama umejaliwa mvuto mbele za watu na ukawa unakubalika, basi hiyo ni fursa ya kuweza kufanya biashara kwa kufanya marketing ya biashara za watu wengine au biashara yako binafsi.


5. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani halafu badili hiyo kuwa fursa, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenu au eneo lolote ambalo unatembelea.
  • Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
  • Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
  • Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
  • Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

6. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, unaweza angalia fursa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

7. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara.

8. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI?
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kadhalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi.

9. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza

10. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala nzuri sana za kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku hizi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango wa kutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

11. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika.

12. TUMIA NJIA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA BIASHARA
- Maonyesho ya biashara
- Magazeti,
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
- Kwa marafiki.

13. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako. Na hii unaweza kufanikiwa kwa kuangalia matatizo yanayoikabili jamii hivyo unaweza kuja na ugunduzi utakaoleta suluhisho kwa jamii

SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUPATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA