ALIYEKIRI KUUWA WATOTO 10 NA KUWATOROKA POLISI AUWAWA BAADA YA KUPIGWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALIMtuhumiwa aliyekiri kuwauwa watoto 10 na kunywa damu zao na kisha kuwatoroka polisi ameuwawa kwa kupingwa na wananchi wenye hasira kali.

Mtuhuiwa huyo anaejulikana kwa jina la Masten Wanjala ameuwawa katika kijiji cha Bungoma magharibi mwa Kenya.

Masten alitoroka kutoka  polisi katika mji mkuu, Nairobi saa chache kabla ya kwenda kusikiliza mashtaka yake ya mauaji ya wavulana 14.

Maafisa watatu wa Jeshi la polisi  nchini humo ambao waliokuwa kazini siku hio walifishwa mahakamani siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya kumsaidia mtuhumiwa huyo kutoroka.

Naibu kamishena wa kaunti ya Bungoma Cornelius Nyaribai amethibitisha kifo chake katika ujumbe aliouandikakatika mtandao wa Twittter.