Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe
Dkt Saada Mkuya Salum amezishauri taasisi za Serikali na binafsi zinazotoa
huduma kwa jamii kutoa kipaombele kwa Watu wenye mazingira maalum wakiwemo Watu
wenye Ulemavu wa Uziwi
Dkt Saada ameyasema hayo wakati akiyafungua mafunzo
maalum ya lugha ya alama kwa watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF yaliyoaandaliwa
na Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo
Ameipongeza ZSSF kwa kuwa mfano bora kwa mashirika ya
serikali kuonesha kwa vitendo na dhamira njema ya kuwahudumia wananchi wa makundi
yote kwa kuanza na lugha ya alama ambayo itawasaidia viziwi kupata huduma
wanazozitoa kwa uhakika bila ya gharama ya kutafuta mkalimali
Aidha Dkt Saada ameiomba ZSSF wasiishie hapo bali kutafuta na njia nyengine ya kuwasaidia Watu wenye Ulemavu wa
Uoni kwa kuangalia uwezekano wa kutengeneza kadi za ZSSF zenye alama ya nukta nundu
“Naziomba na taasisi za Serikali ili tuwe na jamii
shirikishi basi sasa hata vitabu vya sera na sheria na vyenginevyo tuhakikishe
tunaandika kwa nukta nundu ili wenzetu wenye Ulemavu wa Uoni nao waweze kusoma
maendeleo ya nchi yetu mfano nzuri tulivyoanza Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais
Bajeti ya Serikali tuliwazingatia kwa kutoa vitabu vilivyoandikwa kwa kutumia
nukta nundu”
Kufanya hivyo kutahusisha huduma wanazozitoa kuwa bora
zaidi na zinazokwenda na wakati huu wa ukuwaji wa teknologia pamoja na kuziomba
taasisi nyengine kujipanga ili ziweze kutoa huduma kwa ufanisi bila ya kuwaacha
wengine kama Watu wenye Ulemavu
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la
Watu wenye Ulemavu linatambua kuwa fursa mpya ya uchumi wa buluu ni kwa ajili
ya maendeleo ya wananchi wote wa Zanzibar hivyo imejipanga kuandaa mpango
mkakati wa kuona lugha ya alama inapewa kipaumbele kufundishwa kwenye taasisi
zote zinazotoa huduma kwa jamii
Nae Mkurugenzi wa Baraza la Watu wenye Ulemavu Mhandisi
Ussy Khamis Debe amesema mafunzo ya lugha ya alama yameanzishwa baada ya kuonekana
kuna upungufu kwa taarifa kwa Watu wenye Ulemavu wa Uziwi
Mhandisi Ussy amesema kati ya changamoto wanazozipata
Watu wenye Ulemavu wa uziwi kutopata taarifa sahihi kwa wakati muafaka na ndio
maana Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu likaamua kuendelea kutoa elimu hii
ya lugha ya alama kwa taasisi tofauti
Mafunzo kama hayo pia hutolewa na Jumuiya ya
wakalimani wa lugha ya alama JUWALAZA, Chama cha Viziwi Zanzibar CHAVIZA na
chuo cha SUZA, hii ni awamu ya pili ya muendelezo wa mafunzo ya lugha ya alama
kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar.