WALIMU WATAKIWA KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO KAZINI

 

Uploading: 1304604 of 1304604 bytes uploaded.

Walimu wametakiwa kuendeleza umoja na mshikamo Katika kazi ili kuipeleka mbele elimu visiwani Zanzibar .


Hayo ameyasema Katibu mkuu Wizara  ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Ali Khamis Juma Katika sherehe ya kuagwa kwa walimu waliostaafu wa skuli ya Sekondari Kwamtupura huko katika ukumbi ya ZSSF Michenzani Mall Mkoa wa Majini Maghari Unguja.

Amesema walimu ndio wenye dhamana kubwa Katika kuhakikisha wanafunzi wanafika mbali kimaendeleo.

Aidha amewasihi wastaafu hao kuyatumia vizuri mafao yao ili kuendelea kujikwamua kimaisha.

Hata hivyo Katibu Ali ameahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto za skuli hio ndani ya miezi 6 ili wanafunzi waendelea kupata elimu bora.

Kwaupande wake MWALIMU mkuu wa skuli ya Sekondari Kwamtupura bi.Ghanima  Ali Abdallah ameupongeza mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF kwa kuwaunga mkono katika shuhuli hio na kuifanya ifane.

Pia ameongeza kusema kuwa hawawezi kuwasahau daima kwa mchango mkubwa uliotolewa na wastaafu hao. 

Nae Mwanasheria kutoka ZSSF ndugu  Ramadhani Juma Suleiman amewataka wastaafu hao kuwekeza mafao yao Katika miradi inayostahiki ili kuendelea kujipatia kipato.

" wastaafu wengine wamekuwa wakijiingiza Katika miradi isiyostahiki Mara baada ya kustaafu hali inayopelekea kurudi nyuma kimaendeleo"

Jumla ya walimu wawili na mlinzi mmoja kutoka skuli ya Sekondari Kwamtupura ambao wanastaafu wameaga leo.