WASTAAFU WA MFUKO WA HIYARI WA ZVSSS WAPOKEA MAFAO YAO

 Jumla ya wastaafu 10 wa mfuko wa uchangiaji kwa hiyari wa Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZVSSS wamepokea mafao yao ya kustaafu.Akimuwakilisha Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Mkuu wa kitengo Cha huduma kwa wateja Bw. Khamis Filfil Thani huko katika kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo Mjini Zanzibar, amesema katika kukamilisha wiki ya huduma kwa wateja Dunia ZSSF ikaona ni vyema kuunganisha na utoaji wa mafao kwa wanachama ambao wamefikia uri wa kustaafu  .

Aidha Bw. Khamis amewataka wastaafu hao kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi ambao hawajajiunga na mfuko huo wa uchangiaji kwa hiyari.

Nae mtaafu wa mfuko huo Be. Ridhwan Bakari ameishukuru ZSSF kwa kutoa mafao Hayo kwa wakati na kushajihisha wananchi kujiunga na Mfuko huo wa hiyari ambao humuwezesha mtu kujiwekea hakiba hata asipokuwa na ajira ya Serikali.


Mfuko wa uchangiaji kwa hiyari wa ZVSSS una takriban wanachama elfu kumi ambopo kila wananchama anapofika umri wake wa kustaafu hupatiwa mafao yake.