ZSSF YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIAWananchi wametakiwa kuendelea kuuamini Mfuko wa hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na kuendele kujiunga kwa wingi.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Muendeshaji wa mfuko huo Bw. Nassor Ahmed Ameir wakati akizungumza na vyombo vya habar huko ofisini kwao Kilimani Mjini Zanzibar.

Amesema kila ifikapo mwanzo wa mwezi wa Oktoba Dunia huadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo kwa mwaka huu Mfuko huo umeadhimisha siku hio kwa  kufanya Mambo mbalimbali ikiwemo kuhakiki kadi na taarifa za wanachama pamoja na kufungua matawi katika kila mikoa " ZSSF inatarajia kufungua matawi ya kutoa huduma katika mikoa mbalimbali ya visiwa vya Zanzibar ili kuondoa usumbufu kwa wanachama wake na ndani ya wiki hii tutafungua tawi ndani ya Mkoa waUnguja "

Akizungumza kwa niaba ya wanachama mstaafu Ramadhani Fatawi Issa wapongeza ZSSF kwa kutoa mafao ya kustaafu ndani ya siku 15 Hali iliyoondoa usumbufu kwa wastaa.


Wiki ya huduma kwa wateja dunia huadhimishwa kila ifikapo wiki ya mwanzo ya mwezi na kwa ZSSF huu Ni mwaka wa nne kuadhimisha siku hii ambapo Mkurugenzi muendeshaji wa mfuko huo ameshuka chini na kuhudumia wateja na kuskiliza changamoto zao ambapo maadhimisho hayo yataendelea kwa siku 8 na yanatarajiwa kumalizikza tarehe 10 mwezi huu.