ZSSF YAFUNGUA OFISI ZAKE NDANI YA MKOA WA KUSINI UNGUJA
Katika muendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja Duniani Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF umefungua ofisi zake katika Mkoa wa Kusini ili kusogeza huduma karibu na wanachama wake na kuwaondoshea usumbufu.


Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kusini ambae pia Ni Mgeni Rasmi wa hafla hio Bw. Rashid Makame Shamsi amesema kufunguliwa kwa tawi hilo ni hatua za kimaendeleo kwani ZSSF ni mfuko unaowakomboa wafanyakazi wanaostaafu kwa kuwapatia mafao..

Aidha DC. Rashid amewaahidi watendaji wa ZSSF kuwapatia mashirikiano ili kuuwezesha mfuko huo kufikia malengo yake yaliyokusudiwa.

Akitoa maelezo mafupi kuhusu ufungunzi wa kituo hicho Mkurugenzi Muendeshaji wa mfuko huo Bw. Nassor Shaaban Ameir amesema ufunguzi wa ofisi hizo katika Mkoa wa Kusini ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi katika ziara zake, kuzitaka taasisi zinazotoa huduma za kijamii kusogeza huduma Kar ibu na Wananchi.

Nao  wananchi wa Wilaya ya Kusini wamesema kufunguliwa kwa ofisi hizo kumewaondoshea ufumbufu wa kufata huduma hizo mjini.

Ofisi hizo za ZSSF ndani ya Mkoa wa Kusini inatarajiwa kutoa huduma kwa zaidi ya wananchama 3000 wailaya ya kusini na Wilaya jirani.