BENKI YA KCB YANG'ARISHA ZANZIBAR BLUE ECONOMY MARATHON 2021

 

Katika kusherehekea mwaka mmoja wa kuwa madarakani rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr Hussein Mwinyi benki mbali mbali zimeungana katika kudhamini Zanzibar Blue Economy Marathon 2021 iliofanyika katika uwanja wa Amani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Banki Cosmas .T. Kimario amesema kuwa wao Kama KCB wataendelea kuungana na Serikali katika sauala zima la kuendeleza Uchumi wa buluu ambapo kwa miaka mitatu iliopita tayari wamewezesha miradi yenye thamani ya takribani ya milioni 60 na bado wanaendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali mbali mbali.

"Miaka miwili iliopita KBC ilikuja na programu TUJIAJIRI ambapo Program hiyo inasapoti vijana,kina mama pamoja na Wajasiriamali wadogo wadogo".amesema Mkurugenzi huyo

Ameongeza kuwa benki ya KCB tayari imetoa mafunzo, mitaji kwa wajasiriamali na Sasa wanaendelea na programu nyengine ambapo Wajasiriamali wengine miambili wanatarajiwa kupewa mafunzo ya ujasiriamali wa Mambo mbali mbali.

Pia amemalizia kwa kumpongeza rais Dr Mwinyi kwa kufikisha mwaka mmoja katika uongozi wake na kumtakia Kila la kheri katika uongozi wake.

Katika mbio hizo benki ya KCB imedhamini km 10