
Mkurugenzi Mkuu wa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Mhandisi Dkt. Samuel
Gwamaka amesema kuwa maeneo ya fukwe au vyanzo vya maji ni maeneo nyeti kimazingira
kwa sababu ni maeneo ambayo yanategemewa na viumbe wa Baharini na Jamii
inavitegemea.
Ameyasema hayo
alipofanya ziara pamoja na wakaguzi wa mazingira kutoka NEMC katika maeneo ya
fukwe za Coco jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hiyo ni kwa ajili ya ukaguzi
wa mazingira katika eneo hilo.
Aidha, Dkt. Gwamaka
ameeleza kuwa ziara hiyo katika maeneo ya Fukwe za Coco ni kutokana na ujenzi
au maendeleo yanayofanyika katika eneo hilo kuangalia kama yamezingatia Sheria
ya Mazingira 2004 ambayo inasema maendelezo yoyote ambayo ni ya kudumu au
ambayo yanaweza kuleta athari zozote za kimazingira basi yafanyiwe Tathmini ya
Athari ya Mazingira.
ameendelea kusema
"mazingira ya fukwe za Coco kwa sasa yanaridhisha kutokana na ujenzi wa
majengo ya muda yanayovutia yaliyojengwa maeneo hayo ambayo yanatoa nafasi kwa
wajasiliamali wenye kipato cha chini kujipatia fedha za kujikimu pamoja na watu
kupata sehemu nzuri ya kupumzika na kuweza kula. Pia nimpongeze Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
pamoja na uongozi wake wote kwa jitihada wanazofanya kuwatengea maeneo
wajasiliamali wadogo na vilvile kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa utaratibu
maalum kama ambavyo ujenzi wa vibanda visivyo vya kudumu unavyoendelea katika
fukwe za Coco" Dkt.Gwamaka
Dkt. Gwamaka amesema
kuwa watashirikiana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Manispaa ya Kinondoni ilikuona
namna gani wataboresha maeneo hayo ili kukabiliana na changamoto za kimazingira
ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa fukwe unaosababishwa na Mabadiliko ya Tabianchi
kwa hiyo mahali hapa panatakiwa kufanyiwa maboresho kwa kuweka mawe ambayo
yatasaidia maeneo haya yawe endelevu pamoja na kuboresha miundombinu ya maji
taka na maegesho ya magari
Amemaliza kwa kusema
kuwa jambo kubwa la kuzingatia maeneo haya ni kuongeza idadi ya vyoo kwani kutokana
na muonekano mzuri wa maeneo hayo basi watu wengi watavutiwa kuja hapa. NEMC
tutakuwa bega kwa bega na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha
mahali hapa panakuwa salama wakati wote ili eneo hili liwe eneo ambalo wananchi
wa kawaida wanaendelea kufaidi matunda ya uhuru wa Nchi, na liwe eneo la mfano
kwa wajasiriamali wadogo kwa nchi nzima ya Tanzania.