KVZ: ITAKAVOKUJA NDIVYO TUTAKOVOCHEZA NAYO

 Kocha wa timu KVZ Hussein Ramadhan amesema kuwa wamejipanga kupambana katika mchezo wao wa ligi kuu soka Zanzibar na kuondoka na ushindi wa alama tatu dhidi ya Machomane.


Pambano hilo Iikiwa ni muendelezo wa ligi hiyo ambayo itapigwa majira ya saa 10:00 huku mchezo huo ukitarajiwa kua na ushindani mkubwa kutokana wapinzani wao wanahitaji kuonja laza ya ushindi lakini kvz nao wanaohitaji ushindi.

Ameongeza kuwa mchezo wao na Machomane utakua ni mchezo wenye ushindani mkubwa kwavile anajua anacheza na timu ambayo ina ari lakini anajua vipi ataijeruhi Machomane ili aweze kutoka na pointi tatu za mchezo huo

Ameongeza kuwa katika zile namna tatu za ulinzi yeye atatumia moja atacheza kwa kumshambulia zaidi mpizani wake ili asipate nafasi ya kuishambulia KVZ. amesema Kocha wa kvz

Nae kepteni wa timu ya Kvz Suleiman Abdi Juma amesema mchezo wao na Machomane utakua ni mchezo mgumu lakini wao Kama wachezaji watapambana kutoka ushindi.

Ameongeza kuwa timu ya Machomane ni timu ambayo inapambana na ina ari kubwa na inaushindani mkubwa kwavile baadhi ya Wachezaji wametoka KVZ na wanacheza Machomane.

Kwaupande wake Kocha msaidizi wa Machomane Salim Kivumbi amesema kuwa KVZ ni timu kubwa napia ni timu kongwe wanawaheshimu wanajua wamepoteza mechi mbili na matokeo ya mpira Kuna kushinda na kushindwa hayo yote ni matokeo na Sasa wanaangalia linalokuja.amesema Kocha Kivumbi

Amemalizia kwa kusema kuwa wameyaona makosa yao na wapo katika kuyafanyia kazi ili yasijirejee.amesema Kocha Kivumbi

Nae kepteni wa Machomane Seif Ali Hamad amesema mechi yao na kvz itakua ni mechi ngumu hasa wanapokutana na KVZ

"Mpira hauna zama, zama za nyumazimemaliza kesho tunakutana nao tena kwa mara ya tatu na mchezo wetu na kvz ni sheria kupata pointi tatu"amesema kepteni wa Machomane.

Mchezo huo utasukumwa kesho saa 10: katika kiwanja Cha Amani.

Story na Ruwaida Saleh .