Waziri Wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, Amewataka wafanya kazi wa Sekta ya Afya na wananchi kuisaidia Serikali kuokoa fedha kwa kutumia Hospitali zalizopo Nchini badala ya kwenda kutbiwa katika Hospitali za Nje ya Nchi ambapo hupelekea Serikali kutumia fedha nyingi.
Alisema hayo wakati wa maadhimisho ya sherahe ya SIKU YA MIONZI [RADIOLOGY DAY] Iliyofanyika huko Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, ambapo sherehe hiyo hufanyika kila ifikapo Tarehe 8 mwezi 11 kwa kila mwaka.
Aidha Waziri, Mazrui alifahamisha kuwa kituo cha Hospitali kuu cha Mnazi Mmoja ni kituo cha kujifunzia kwa Wataalamu mbali mbali wa ndani na njea ya nchi kwani sasa kina wataalamu wazuri walio bobea katika taaluma ya afya na vifaa vingi vya kisasa.
Pia aliwanasihi Madaktari kutowauzia huduma za afya wagonjwa kwani kufanya hivyo husababisha kupata laana za wangonjwa na kupelekea wananchi kuilaumu Serikali jambo ambalo sio sahihi na kinyume na maadili ya kazi.
Vilevile aliwasisitiza Madaktari kutovunjika moyo na kufanya kazi kwa moyo mmoja kwani Serikali inatambua kuwepo kwa changamoto ambazo wanakabiliana nazo wataalamu wa kitengo cha RADIOLOGY katika hospitali mbali mbali .
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Daktari Msafiri Marjani, aliwaomba wataamu wa mionzi kuwafikishia waananchi taaluma hii juu ya faida na hasara zinazopatikana katika vipimo hivyo.
Hata hivyo aliwanasihi wananchi kuacha tabia ya kupiga mionzi mara kwa mara bila ya kuwa tatizo kubwa ambalo litalazimu kufanya vipimo hivyo kama vile EXRAY na CT SCAN kwani vipimohivyo vina mionzi mikali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kwa wagonjwa.
Nao wataalamu kitengo hicho walieleza kuwa Kituo cha Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kimeweza kupunguza idadi kubwa ya wagonja wanofika kwa kupatiwa huduma hiyo kutokana na kuwepo na vituo vya huduma hiyo kila Wilaya.
Wafanya kazi hao wameiomba Wizara kuwapatia nafasi za kwenda kusoma kozi za muda mfupi ilikuongeza taalumazaidi kwani elimu inaongezeka kila siku.