ZSSF WAZINDUA MFUMO MPYA WA UWASILISHAJI MICHANGO, WAZIRI SORAGA ATOA NENO KWA WAAJIRIWaajiri wametakiwa kujisajili kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii kuwa wanachama wachangiaji na kuwasajili wafanyakazi wao kuwa wanachama wanufaika wageni na wenyeji. 


Ameyasema hayo Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na uwekezaji Mh. Mudrik Ramadhani Soraga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa wadau wa ZSSF huko Katika ukumbini wa Michenzani Mall Kisonge Mjini Zanzibar.

Amesema mkutano huo ni fursa adhimu ya kupata wasaa wa kukutana na uongozi wa Mfuko, ili kuweza kuona jinsi ya mambo yanavyoendeshwa ndani ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii. Lakini pia kupata fursa ya kutoa maoni ambayo yatakuwa chachu ya maendeleo ya Mfuko.


Aidha Waziri Soraga amewataka ZSSF kuzidisha uelimishaji wa utumiaji wa mifumo ya kieletoniki ili iwe rahisi kutumika, lakini pia kutoa usaidizi wa karibu na kwa uharaka pale watumiaji wa mifumo hiyo watakapohitaji hivyo.

Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa mfuko huo Bw. Nassor Shaaban Ameir amesema lengo la ZSSF unapoanza mwaka 2022 waajiri wote waweze kuutumia mfumo kieletoniki Katika kufanya malipo ili kuendana na lengo la Serikali ya awamu ya nane kuwa malipo yote yafanyike kwa njia hio ili kuepuka udanganyifu na mianya mengine.


Pia amewashajihisha wadau na wananchi wote kujiungeni na ZSSF na kuwasilishe michango sahihi na kwa wakati ili tujenge nchi.

Akitoa neno la shukurani Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini Dk. Huda Ahmed Yussf amesema ZSSF ina njia mbada ya kupokea maoni kwa wanachama wake haswa Katika zama hizi za utandawazi kwa kuweka social media accounts ambzo kila mwananchi anaweza kutoa maoni yake.


Kwaupande wake mshiriki wa mkutano huo kutoka Bastart limeted bi Safia Ibrahim Mohd ameipongeza ZSSF kwa kuelimishe waajiri na wafanyakazi umuhimu wa kujiwekea hakiba pia kuweke muda wa kukutana na wadau na kusikiliza changamoto zao.


Mkutano huo wa sita wa wadau wa ZSSF umeendasambamba na uzinduzi  rasmi wa Mfumo wa uwasilishaji wa michango ya waajiriwa yaani  (ZSSF EMPLOYERS SELF SERVICE WEB PORTAL) pamoja na utoaji zawadi kwa tasisi zilizofanya vizuri na makundi yaliosaidia maendeleo Mfuko wa hifadhi ya Jamanii zanzibar.