ZSSF YAWAPA MBINU WASTAAFU YA KUPAMBA NA WIZI WA KIMITANDAO

 


Wastaafu wametakiwa kuwa waangalifu na kutumia vyema mafao yao ili yaweze kuwasaidia Katika siku za mbele .Ameyasema hayo  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Haroun Ali Suleima kwenye mafunzo kwa wastaafu watarajiwa wanaolipwa na ZSSF huko Katika ukumbi wa Michenzani Mall kisonge Mjini Zanzibar amesema.

Kustaafu sio mwisho wa maisha hivyo ni vyema kujianda  Katika maisha yao mpya baada ya Utumishi.

Pia Mwalim Haroun amewataka ZSSF kuwawahishia wastaafu mafao yao kwani wamelitumikia Taifa kwa siku nyingi.

Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Bw. Nassor Shaaban Ameir amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwaandaa wastaafu hao kisaikolojia ili kuweza kupambana na changamoto baada ya kustaafu.


Aidha amesema ZSSF imepiga hatua kubwa Sana kwa kuunganisha mifumo wa kieletroniki ya kutunza kumbukumbu za michango ya wastaafu ili kuondoa usumbufu pindi wanapostaafu.
   
Akizungumza kwa niaba ya wastaafu Bw. Talib Juma Ali amesema Mafunzo hayo yamewasaidia kupata maarifa ya kutumia mafao yao vizuri kwani kumekuwa kesi nyingi za upoteza fedha za kiinua mgongo mara baada ya kustafu kwa kuwekeza kwenye miradi isiyofaa.

Mafunzo hayo yaliyowashirikisha wasstafu watarajiwa ni ya nne kufanywa na Mfuko wa hifadhi ya jamani Zanzibar ZSSF kwa miaka tofauti Unguja na Pemba ambayo hufanyika kila mwezi November ya kila mwaka.