MASHIDANO YA MPIGA PICHA BORA WA SLR WAPATIKANA WASHINDIFainali ya mashindano ya SLR yalioandaliwa na CapeTown Fish Market kwa kushirikiana na Robin Batista tayari yamekamilika kwa kutoa jumla ya washindi 10 katika vipengele tofauti tofauti ikiwemo na champiga picha maarufu wa Mji Mkongwe.

Mashindano hayo ambayo yanalengo la kukuza vipaji vya wapiga picha wenyeji ambapo hii ni mara ya Kwanza kwa Kampuni ya Cape Town Fish Market kuandaa Machuano hiyo.

Kampuni ya Cape Town Fish Market kwa kushirikiana na Batista wameahidi kuwa wataendelea kuandaa Mashindano Kama hayo kwa Waasili kwa lengo la kurejesha shukrani kwa jamii inayowazunguka.

Jumla ya washiriki 10 wamechaguliwa ambao kuwania vipengele mbalimbali kwenye mashindano hayo ambao ni:-
1) Keegon J. Checks
2)Mohammed Ali
3) Ali Hasnein
4) Aisha Suleiman
5) Prerna Surt
6) Haji Masoud
7) Stephen Kilonzo
8) Ashraki Mussa
9) Hamed Mohamed
10) Khudaija Hasnein
Na washindi walikua wanne
Mshiriki Khudaija Hasnein amefanikiwa kupata nafasi ya kwanza ( Pollution in my playground ) na Hamed Mohamed kushika nafasi ya pili ( I am flying) huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Ashraki Mussa (Breaking boundaries ) na nafasi ya nne imerudi tn kwa Hamad Mohamed( The most promising photographer)