MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF) UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOLIPWA PENCHENI YA ZSSF KUWA ZOEZI LA UHAKIKI WAO WA MWANZO WA MWAKA SASA UTAFANYIKA KUANZIA JUMATATU YA TAREHE 03/01/2022 HADI JUMAPILI 09/01/ 2022.
KWA WASTAAFU WA UNGUJA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KWA UTARATIBU UFUATAO:-
TAREHE :
03 JANUARI HADI 09 JANUARI 2022
MUDA : KUANZIA SAA 2:00
ZA ASUBUHI MPAKA SAA 7:00
MCHANA
PAHALA:
KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO KARIAKOO.
AIDHA KWA KUWAPUNGUZIA USUMBUFU
WASTAAFU WALIOPO MASHAMBA, UHAKIKI HUO PIA UMESOGEZWA KARIBU NA MAENEO
WANAYOISHI KAMA IFUATAVYO:-
Ø KWA
WASTAAFU WA KASKAZINI UNGUJA
WANATAKIWA KUFIKA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA KUANZIA TAREHE 03/01/2022 HADI
TAREHE 04/01/2022
Ø KWA
WASTAAFU WA WILAYA YA KATI
WANATAKIWA KUFIKA KITUO CHA WAALIMU TC DUNGA KUANZIA TAREHE 05/01/2022
HADI 06/01/2022
Ø KWA
WASTAAFU WA WILAYA YA KUSINI UNGUJA
WAFIKE KITOGANI KATIKA AFISI ZA HALMASHAURI KUANZIA TAREHE 07/01/2022 HADI 08/01/2022
KWA WASTAAFU WA PEMBA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA:-
TAREHE
: 03 JANUARI HADI 09 JANUARI 2022
MUDA : KUANZIA
SAA 2:00 ZA ASUBUHI MPAKA SAA 7:00
MCHANA
PAHALA : AFISI ZA ZSSF TIBIRINZI
CHAKECHAKE PEMBA.
Ø KWA
KASKAZINI PEMBA, WASTAAFU WANATAKIWA
WAFIKE JAMHURI HALL WETE TAREHE 03 HADI TAREHE 04/01/2022.
Ø NA
PIA UKUMBI WA SHAAME MATTA MICHEWENI KWA TAREHE 05 HADI 06/01/2022
Ø NA
KWA KUSINI PEMBA, WASTAAFU
WANATAKIWA KUFIKA AFISI YA BARAZA LA MJI MKOANI KUANZIA TAREHE 07/01 HADI 08/01/2022
AIDHA KWA WASTAAFU WALIOPO DAR ES SALAAM UHAKIKI WAO UTAFANYIKA:-
TAREHE:
03/01/2022 HADI 07/01/2022
PAHALA: AFISI
ZA IDARA YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ
ZILIZOPO MTAA WA LITHULI
MKABALA NA JENGO LA
WIZARA YA FEDHA YA JAMHURI YA
MUUNGANO WA
TANZANIA
MUHIMU
KUZINGATIA:-
1. WASTAAFU
WATAKAPOKWENDA KUHAKIKIWA WANATAKIWA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO VYA USTAAFU VYA
ZSSF NA ASIYEHAKIKIWA PENCHENI YAKE ITAZUIWA.
2. WAHUSIKA
WANAOMBWA KUFUATA WAKATI NA SIKU HIZO ZA UHAKIKI KAMA ZILIVYOPANGWA.
3. UHAKIKI
WA WASTAAFU HAUTAFANYWA KATIKA AFISI ZA KILIMANI MNARA WA MBAO
4. WASTAAFU
AMBAO NI WAGONJWA AU WASIOJIWEZA WANAOMBWA KUBAKI NYUMBANI. WATEGEMEZI AU
WASAIDIZI WAO WAWASILISHE KADI ZAO KWA AJILI YA KUHAKIKIWA.
KILA ATAKAESIKIA TANGAZO HILI ANAOMBWA
AMUARIFU MWENZIWE.
ZSSF NI UFUNGUO WA MAISHA
YA BAADAE!!!
TANGAZO
HILI LIMETOLEWA NA:
KITENGO CHA
MASOKO NA UHUSIANO
MFUKO WA HIFADHI
YA JAMII ZANZIBAR - ZSSF