ZSSF KARIAKOO FESTIVAL 2021 YAZINDULIWA

 


Wajasiriamali wametakiwa kutumia fursa za maonesho kujitangaza na kutafuta masoko ili kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha.


Ameyasema hayo Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dkt. Islam Seif Salim  wakati wa tamasha la wajasiriamali la ZSSF KARIAKOO FESTIVAL 2021  huko katika kiwanja Cha kufurahishia Watoto Kariakoo Mjini Zanzibar .

Amesema Maonyesho hayo yamesaidia Serikali Katika kuwakwamua wajasiriamali kiuchumi kwani wanapata fursa ya kujikusanya na kutangaza bidhaa zao.

Aidha amewasihi wajasiriamali kujiandikisha na kuchukua vitambulisho vya wajasiriamali wadogowadogo vilivyotolewa na Serikali ili kupata manufaa makubwa kwani Serikali ya awamu ya nane ina dhamira ya kuwakomboa.


Sambamba na hayo amesema Wizara ya biashara na maendeleo ya viwanda itaendelea kuunga mkono juhudu zinazofanywa  na ZSSF Katika Katika kuwanyanyua wajasiriamali ili kupunguza umasikini nchini.

Kwaupande wake Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF amesema tamasha hilo ni la nne toka kuanzishwa kwake ambapo wajasiriamali hupata fursa ya kujifunza kwa kupatiwa elimu  na kutangaza biashara zao ikiwa ni sehemu ya kuwapatia masoko.


Pia amewashajihisha wajasiriamali kujiunga na mfuko wa hiyari wa ZVSSS ambao unatoa mafao tofauti ikiwemo mafao ya elimu,ulemavu na uzazi.


Tamasha la 4 la ZSSF KARIAKOO FESTIVAL limeandaliwa na mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar Kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda limezinduliwa rasmi leo  Disemba 13 ambalo litaendelea kwa siku 10 na kudhaminiwa na NHIF, AMANA BANK, MKOANI HOTEL ZANZIBAR, BANK OF AFRICA na ZVSSS ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni " Wekeza na ZSSF kwa maisha ya uzeeni "