WASTAAFU WAIPONGEZA ZSSF KWA KUIMARISHA HUDUMA KWA WANACHAMA WAKEWastaafu wanaopokea pesheni zao katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wameupongeza Mfuko huo kwa kuwasogezea huduma karibu ambayo imewasaidia kuwaondolea usumbufu wa kuifata Mjini.


Wakizungumza katika muendelezo wa uhakiki baadhi ya wastaafu waliofika katika ofisi za ZSSF Kitogani Mkoa wa kusini Unguja Wamesema kuwepo kwa ofisi za ZSSF ndani ya Mkoa huo kumerahisishia wanachama kupata huduma zote  kwa urahisi badala ya kuzifata mjini.

Aidha wamesema wamewasihi waajiri kuwaunga wafanyakazi wao katika mfuko huo kwani humsaidia mtu mara baada ya kustaafu.

Kwaupande wake mkuu wa vituo vya uhakiki mkoa wa kaskazini na kusini Unguja Bw. Omar Nasib Ramadhan Amesema ZSSF katika kusogeza huduma wanachama wake inafika katika tasisi mbalimbali kutoa huduma za mfukoa huo pia kuwafata wastaafu waliowagonjwa majumbani kwaajili ya kuwahakiki.

Jumla ya wastaafu 13,548 wanaopokea pensheni zao katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wanatarajiwa kufanyiwa uhakiki katika Mkoa wa kaskazini, Mkoa wa kusini pamoja na Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.