ZSSF WAZINDUA MFUMO WA KIELETRONI WA KUHIFADHI NYARAKA NA MAJALADA YA WANACHAMA WAKE

 


Katika shamrashamra za kuadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF umezindua mfumo wa usimizi wa nyaraka na majalada ya kieletronik ( ELECTONIC DOCUMENT MANAGEMENT & ARCHIVING SYSTEM- EDMAS ).


Akisoma hotuba yake kwenye uzinduzi huo Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mh. Suleiman Masoud Makame huko katika ofisi za ZSSF Kilimani mnara wa mbao Mjini Zanzibar amesema mfumo huo ni wa kwanza kwa Zanzibar ambao unihifadhi majalada na nyaraka za kila mwanachama hivyo ni vyema kila mmoja akawa ni mlinzi kwa mwenziwe pia kuondoa muhali kwa yoyote atakaefanya uharibifu.

Aidha ameipongeza ZSSF kwa kutekeleza kwa vitendo azma ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi na kuthibitisha kuwa Zanzibar inaweza kuwa na mfumo huo.

Akitoa maelezo ya mfumo huo wa  EDMAS kwaniaba ya Katibu Mkuu, Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Bw. Rashid said Rashid amesema mfumo huo ni mjumuisho wa teknolojia mbalimbali ambazo zinafanya kazi kwapamoja ili kutoa suluhu Katika kutatua changamoto za usimamizi wa uhifadhi wa majalada, nyaraka na kumbukumbu Katika mfuko wa hifadhi ya jamii.


Hatahivyo amesema mfumo huo utasaidia wanachama kupata taarifa haraka zaidi, kuzibiti upotevu wamajarada, kupunguza  gharama za uendeshaji kwa mfuko kwa kuondoa matumizi ya karatasi kadhalika kurahishisa utoaji wa taarifa kwenda kwenye tasisis nyengine  za serikali wakati wa uhitajiwa vielezo.Ufunguzi huo wa mfumo wa usimizi wa nyaraka na majalada ya kieletronik ( ELECTONIC DOCUMENT MANAGEMENT & ARCHIVING SYSTEM- EDMAS ) umegharimu jumla ya shilingi milioni 765.7 hadi kukamilika kwake ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.