ZSSF YATARAJIA KUHAKIKI WASTAAFU 600 MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

 

 


Jumla ya wastaafu 600 wanaopokea pencheni zao katika mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF wanatarajiwa kuhakikiwa taarifa zao katika Mkoa wa kaskazini Unguja.


Akizungumza katika kituo Cha Mahonda mkuu wa vituo vya uhakiki Mkoa wa Kusini na kaskazini Unguja Bw. Omar Nasib Ramadhani amesema Hadi kufikia Sasa zoezi hilo linakwenda vizuri ambapo takribani ya wastaafu 400 tayari wameshahakiki taarifa zao .

Aidha amesema lengo kuu la uhakiki huo ni kukabiliana na changamoto ya kuwaondoa wastaafu hewa na kujua idadi sahihi ya wastaafu waliingia na waliotoka ( waliofariki ).

Hatahivyo Mkuu huyu amesema ZSSF inamatarajio ya kufungua tawi lake jipya katika Mkoa wa kaskazini ndani ya mwezi huu wa January 2022 ili kuendelea kuboresha huduma zao na kuondolea usumbufu wanachama kwa kuwasongezea huduma karibu.

Nao wastaafu waliohakiki taarifa zao waeiomba ZSSF kuwaongezea fungu katika fedha zinazopatika kwenye miradi mbalimbali wanayowekeza.
 
" Zoezi la uhakiki zuri watoa huduma amehipanga vizuri tunapofika tunahudumiwa na kuondolea Ila tunaomba na sie tuengezewe chochote kwenye miradi inayowekezwe " Bw. Mohd Ali Haji ( mstaafu wa ZSSF )


Zoezi la uhakiki kwa wastaafu hufanyika kila mwezi wa kwanza na mwezi wa Saba kila mwaka ambapo kwa Mkoa wa Mjini kituo ni kiwanja Cha kufurahishia Watoto Kariakoo na kwa Mkoa wa kaskazini kituo ni kiwanja Cha sukari Mahonda.