ZSSF YAWAHIMIZA WASTAAFU KWENDA KUHAKIKI TAARIFA ZAOWachama wanaopokea penchezi zao Katika  mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF wametakiwa kujitokeza kwa wingi Katika zoezi la uhakiki ili kuendelea kupata pencheni zao bila usumbufu.Wito huo umetolewa na mkuu wa vituo vya uhakiki Mkoa wa Kaskazini na Mkoa wa Kusini Unguja Bw. Omar Nasib Ramadhani huko Katika kituo Cha walimu TC Dunga Wilaya ya Kati 


Amesema uhakiki unasaidia kuimarisha utoaji wa pencheni  kwani baada ya zoezi hilo wa ZSSF inaende kuweka pencheni zao .


Aidha amesema kwenye Mkoa wa Kusini ZSSF inatarajia kuhakiki takribani wanachana 900 ambapo Hadi sasa zaidi ya wanachama 300 tayari wameshahakikiwa Katika kituo Cha walimu TC Dunga Wilaya ya Kati.


Kwa upande wao wastaafu waliofika kufanya uhakiki wameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuweka mfuko ( ZSSF ) wa hifadhi ya jamii ambao humsaidia mwanachi kujikwamua kimaisha baada ya kustaafu.


Sambamba na hayo wameiyomba ZSSF kuendelea kuboresha huduma zao ili wazidi kunufaika na mfuko huo pia kuwahamasisha wenanchi wengine kujiunga.


Zoezi la uhakiki kwa wastaafu wanaopokea penchezi zao Katika mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF ambalo limeanza tarehe 3 January 2022 bado linaendelea Katika vituo vyake vya Mkoa wa Mjini na mkoa wa Kusini.