ZSSF YAFANYA UHAKIKI KWA WANACHAMA WAKE, YAANZA NA TASISI ZA SERIKALI

 

Waajiri wametakiwa kutoa taaarifa mapema Kwa wafanyakazi wao pindipo wanapopokea taarifa ya uhakiki Ili kurahisisha zoezi.

Wito huo umetolewa na mkuu wa kitengo cha kumbukumbu ZSSF bi Zainab Rajab Baraka wakati wa zoezi la uhakiki Kwa wafanyakazi wa tasisi za Serikali huko katika ukumbi wa Idris Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Amesema uhakiki huo utasaidia kukusanya taarifa za wanachama na kuziweka sawa Ili kurahusisha kupata mafao yao mapema wakati wakistaafu.

Aidha Bi Zainab amesema jumla ya tasisi 40 za Serikali tayari wamezipelekea taarifa za kufanya uhakiki ambapo Kwa Leo wameanza na Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais na Ofisi ya Rais Fedha na mipango.

Akizungu mara baada ya kuhakiki taarifa zake Mkurugenzi Baraza la taifa la watu wenye ulemavu kutoka Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ussi Khamis Debe amesema zoezi hilo limewasaidia kujua taarifa za michango yao na kujua kama kuna upungufu wa utoaji michango.

Haya hivyo amewashajihisha watendaji wa tasisi nyengine za Serikali na binafsi kujitokeza Kwa wingi wakati wa kuhakiki taarifa zao . 

Zoezi hilo la uhakiki wa wanachama wa mfuko wa hitadhi ya jamii Zanzibar ZSSF umeanza Leo Febuari 28, 2022 Kwa tasisi za Serikali na kumalizia sekta binafisi Kwa lengo la kukusanya taarifa ambazo hazimo kwenye kumbukumbu na kuhakikisha wanapata huduma Kwa wakati.