ZSSF YAFUNGUA OFISI MPYA MKOA WA KASKAZINI UNGUJAWatendaji wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wametakiwa kuhakikisha wanatoa huduma Bora zaidi katika ofisi yao  mpya ya mkoa wa kaskazini ili kuwavutia wanachama wake.


Wito huo umetolewa na  Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Mh. Ayoub Mohd Mahmoud wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Zssf kinduni Mkoa wa kaskazini unguja .


Amesema utendaji wao wa kazi utasaidia kuongezeka kwa wanachama katika Mfuko huo pia utaondoa usumbufu wa kufata huduma Mjini.

  “Iwapo kutakuwa na huduma nzuri hata nawachama wa Mjini watakuja kaskazini  “ amesema RC.Ayoub.

Sambamba na hayo Mh. Ayoub ametoa rai kwa Taasisi nyengine kuiga mfano wa ZSSF kuboresha na karibu na jamii.  .

Akitoa maelezo mafupi ya ofisi hio MKurugenzi muendeshaji wa ZSSF Bw. Nassour Shaban Ameir amesema ufunguzi wa ofisi hiyo ni chachu ya kuongeza wanachama wapya  wa ZSSF  na ZVSSS katika Mkoa huo.


Ufunguzi wa Ofisi hio ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Hussein Ali Mwinyi  kuwawasogeza huduma karibu na wananchi wake .