WAZIRI LELA APOKEA CHEKI YA MILIONI 30 KUTOKA ZSSFKufuatia ajali ya kuungua na moto skuli ya Utaani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyotokea hivi karibuni na kusababusa hasara kubwa Mfuko wa hitadhi ya jamii Zanzibar ZSSF umekabidhi cheki ya sh milioni 30 Kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Kwa lengo la kusaidia janga hilo.Akizungumza mara baada ya kukabidhi cheki hiyo Mkurugenzi muendeshaji wa ZSSF Bw. Nassor Shaaban Ameir  huko katika Ofisi za Wizara hio Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar amesema ni wajibu wa ZSSF kusaidia jamii pale inapohitaji msaada .

Kwaupande wake Waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Mohd Mussa ameipongeza ZSSF kuwa tasisi ya kwanza kabisa kuguswa na janga hilo na kuchagia Fedha.


Aidha amehakikisha kuwa msaada huo utakwenda kusaidia katika ujenzi wa ukarabati wa skuli hiyo ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi6.


Nae naibu Waziri wa Wizara hio Bw. Ali Abdullgulam amesema msaada huo utakwenda kuwa hamasa Kwa tasisi nyengine kusaidia katika janga hilo.Makabidhiono hayo ya cheki yamefanyika leo Mach 17,2022 ambapo  Waziri wa elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Lela Mohd Mussa amepokea cheki hio kwa niaba ya skuli ya Utaani.