WAZIRI SADA MKUYA AFANYA ZIARA ZSSF, ARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WAOMfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF umeshauriwa kubuni mbinu Bora ya kuongeza wanachama wapya katika taasisi mabali mbali ikiwemo sekta binafsi ili kuongeza mapato kwenye mgmfuko huo.


Wito huo umetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dk. Sada Mkuya Salum wakati wa ziara yake ofisini hapo Kilimani Mnara wa mbao Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Amesema bado elimu inahitajika katika tasisi hizo ili zihakikishe zinasimamia wajiriwa wao kujiunga na Mfuko huo amboa ni Mfuko pekee kwa Zanzibar .

Aidha Dk.Sada ameipongeza ZSSF Kwa hatua kubwa ya maendeleo waliofikia Kwa  kuandaa mfumo wa kieletronic ambao utawaondolea usumbufu wanachama kwa kupata huduma kupitia simu zao za mkononi sambamba na kuwataka waimarisha njia Bora ya kutoa huduma ya fao la uzazi kwa kinamama.


Akitoa taarifa kuhusu Mfuko huo Meneja Mipango uwekezaji na utafiti Abdulazizi Ibrahim Iddi amesema Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili ni kukosa mashirikiano na baadhi ya taasisi.


Akitoa Shukrani Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Khadija Shamte Amesema watafanyia kazi ushauri wa Waziri na wataendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii na wawekezaji ili kuhakikisha wanaongeza wanachama katika Mfuko huo .


Ziara hio ya kutembelea mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF ni muendelezo wa zira za  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dk. Sada Mkuya Salum kutembelea tasisi zote zilizo chini ya wizara yake.