ZANTEL YAJA NA NEEMA KWA WAZANZIBARI



kampuni ya simu za mkononi ya Zante kupitia  huduma ya lipa kwa simu imeendeleza huduma ya LIPA NUSU BEI ili kusaidia wananchi wa visiwani Zanzibar kununua bidhaa kwa bei ya chini.

Hayo yamesemwa na Mtaalamu wa Huduma ya Ezypesa wa Zantel Eunice Hubert Alelyo huko katika Soko la Darajani Mkoa wa Mjini  Magharib Unguja.

 Amesema huduma hio itakwenda kuwakomboa wananchi haswa katika kipindi hichi  cha kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo watapata fursa ya kununua vyakula kwa bei nafuu.

Aidha amesema kuwa huduma ya lipa kwa  simu ya Zantel unaweza kutumia kupitia mtandao wowote wa simu na  na kununua chochote.

 Akizungumza mara baada ya kufanya manunuzi ndugu Nassir Ali Mdungi amesema huduma hio imekuja kukomboa wananchi wa Zanzibar kwani ni rahisi kwa wanunuzi na wafanyabiashara.


Maeneo zaidi ya 20 yatarajiwa kufikiwa Zanzibari na kupata huduma ya nusu bei ili kushajihisha wananchi kutumia huduma ya lipa kwa simu na Zantel.