ZANTEL YAZINDUA HUDUMA YA LIPA KWA SIMU.Katika kuboresha huduma za malipo kidigitali, kampuni ya Zantel leo imezindua huduma yake ya Lipa kwa Simu ambayo itawaruhusu wateja kulipia bidhaa na huduma moja kwa moja kutoka kwenye simu kwenda kwa wafanyabiashara.


Huduma hiyo itachochea maendeleo na matumizi ya teknolojia kwenye huduma za malipo kwenye sekta zote za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Afisa Mkuu wa Fedha wa Zantel, Aziz Said Ali alisema huduma hiyo  itasaidia katika kuongeza ufanisi kwa wafanyabiashara pamoja na kuongeza usalama wa fedha kwa wananchi. 

“Huduma hii itaboresha mfumo wa malipo kuwa ya kidigitali zaidi hapa Zanzibar kwani wateja wataweza kulipia bidhaa na huduma kwa kulipa moja kwa moja kutoka kwenye simu zao. Hii inaondoa ulazima wa kubeba pesa taslimu ambazo usalama wake ni mdogo,” alisema. 

Zantel inakuwa kampuni ya kwanza kwa Zanzibar kuanzisha huduma hiyo ambayo ni huduma kamili ya kidigitali inayowaruhusu wateja kulipia kutoka mitandao mingine. 

“Tuna wafanyabiashara zaidi ya 4,000 ambao wanatoa huduma hii kote Unguja na Pemba na tunaendelea kusajili wafanyabiashara wengi Zaidi ili huduma hii ipatikane kila kona ya Zanzibar,”


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza ajenda ya Uchumi wa Bluu ambayo imejikita katika matumizi ya kimkakati ya rasilimali maji ili kuchangia ukuaji wa uchumi. Huduma hii itasaidia kurahisisha ukuaji wa biashara kwenye sekta kama uvuvi na utalii. 

Mkuu wa Huduma za Fedha wa Zantel, Moses Alphonce alisema huduma hiyo ni rahisi kutumia na hivyo kampuni hiyo inaendelea na utoaji wa elimu kwa wananchi ili waelewe umuhimu wake. 

“Ili Kulipa kwa Simu, unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye menyu ya huduma za fedha ya mtandao wako na kufuata maelekezo.Kwa watumiaji wa simu janja wanaweza kulipa kwa ku-scan QR code kwenye App ya Ezypesa,”

Wateja wa Ezypesa watapiga *150*02# na kuchangua 5 Lipa kwa Ezypesa, kisha ingiza Lipa Namba Kisha ingiza kiasi na thibitisha kwa kuweka Pin yako.

Huduma hiyo tayari inapatikama kwenye maeneo mbalimballi ikiwamo Migahawa, hoteli, masoko, supermakets, maduka yad awa, vituo vya mafuta, na maeneo ya wazi kama Forodhani.