ZANTEL YAJA NA RAMADHANI OFFER


Kampuni ya simu za mkononi Zantel imesema itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanaboresha maisha ya wateja wao kupitia huduma bora za mawasiliano ambazo ni za kidigitali zaidi katika nyanja zote.

Kauli hio imetolewa na Mkuu wa Fedha Zantel Bw. Aziz Said Ali wakati wa uzinduzi wa ofa ya Ramadhani ( RAMADHANI OFFER ) huko katika Ofisi zao Amani viwanda vidogovidogo Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Amesema Zantel imeona ipo haja ya kuungana na waislam katika mwezi mtukufu Kwa kuwaletea huduma ambayo itawapa maudhui yanayoendana na Ramadhani Kwa bei nafuu.

Aidha ameeleza maudhui yanayopatikana kwenye ofa hio ni pamoja na Dua, Qaswida, Nasheed, Swala za tarawehe na jumbe za sauti za kujikumbusha muda futari na daku.

Kwaupande wake Meneja wa bidhaa Zantel Bw. Edwin Byampanju amesema ofa hio imezingatia hali halisi ya maisha ya Watanzania Kwa kuziweka gharama nafuu ambapo mteja atalipia sh 100 Kwa siku na kupata taarifa zote ambazo zitamasaidia kukamilisha ibada yake.

Sambamba na hayo Bw. Edwin amewashajihisha wananchi kujiunga ofa hio Kwa kubonyeza 15582 Ili kuimarisha Imani zao haswa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.