ZSSF YAWAFARIJI MAYATIMA UNGUJA NA PEMBA

 Jumla ya shilingi milioni kumi na moja na nusu zimetengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF kwaajili kuwapa sadaka watoto yatika katika mikoa yote ya Unguja na Pemba ambapo hadi sasa tayari Mikoa yote mitatu ya Unguja imeshakabidhiwa msaada huo ikiwemo Mkoa wa Kusini, Kaskazini na Mkoa wa Mjini magharib.

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud akipokea bahasha za sadaka kutoka kwa Afisa uhusiano na masoko kutoka ZSSF Bw. Mussa Yussuf

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohd Mahmoud akimkabidhi mtoto yatima bahasha yenye sadaka.

Meneja wa huduma kwa wateja kutoka ZSSF Bw. khamis filfilthani akimkabidhi bahasha mtoto kutoka kituo cha kulelea watoto yatima cha Kidundo kilichopo Tunguu Wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja.

Meneja wa huduma kwa wateja kutoka ZSSF Bw. khamis filfilthani akiwapatia bahasha za sadaka watoto yatima kutoa kituo cha NASAF EDUCATION CENTER kilichopo Maungani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Rashid Makame Shamsi akimkabidhi bahasha mtoto yatima