TGNP, KAMATI YA UONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAPITISHA MAPENDEKEZO USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI

Baraza la Vyama vya Siasa nchini na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Shirika la WiLDAF kwa ufadhili wa UK Aid wamepisha mapendekezo ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi na uongozi katika Vyama vya Siasa kama sehemu ya uhamasishaji wa utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa. Mapendekezo hayo yamepitishwa leo Juni 13, 2022 huko katika hoteli ya Zanzibar beach resort Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ambapo wajumbe wa mkutano huo wamepitisha hoja na kusema katika kufanikisha hayo watahakikisha kikao kijacho cha baraza hilo kitakuwa na wajumbe wanawake ili kuweka usawa wa kijinsia.Akizungumza Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Mhe. Bw. Juma Ali Khatibu amesema Baraza limepitisha pendekezo la kufutwa kwa gharama zote fomu za wagombea zinazotolewa na Vyama vya Siasa kwa wanawake ili kuongeza ushiriki wa wanawake kujitokeza na kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi.. Pia Baraza limeridhia pendekezo la mabadiliko ya sheria yafanyike ili rushwa ya ngono itambuliwe kuwa mojawapo ya makosa ya uchaguzi kwenye Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kila chama ichukue hatua ya kutengeneza mwongozo na utaratibu wa kutambua viashiria na kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia ndani ya vyama vyao.Aidha Baraza limeridhia maazimio ya kwamba Vyama vya Siasa kutunga Sera za Jinsia kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia (hususan TGNP na WiLDAF) kwa kuzingatia uwepo wa rasilimali fedha, NA KWAMBA mashauriano yafanyike ili kuona namna bora ya kutumia rasilimali ili kutekeleza azma hiyo kwa ufanisi

Hata hvyo wameridhia azimio la kuvitaka Vyama vya Siasa kurekebisha Sera, Katiba na Kanuni ili kuweka Mfumo wa Quota za Hiari na Sera za Jinsia ili kuongeza ushiriki wa Wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi.


Kikao hicho kimekamilika kwa kupitisha maadhimio hayo ya Baraza la Vyama vya Siasa katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa uongozi na ngazi za maamuzi.