TGNP, UONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAJADILI NAMNA YA KUONGEZA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI

 

 Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Shirika la WiLDAF kwa ufadhili wa UK Aid, wamekutana na kamati ya Uongozi wa vyama vya siasa nchini kujadiliana namna bora ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi na Uongozi katika vyama vya siasa kama sehemu ya uhamasishaji wa utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa kipengele cha 6A na 6B. 


 

Kikao hicho kilichofanyika leo Juni 12, 2022 katika ukumbi wa Zanzibar beach resort Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ni mwendelezo wa vikao vya Mashauriano na Baraza vilivyofanyika mwezi Februari mwaka huu ambavyo vilitoka na mapendekezo ya namna ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi. Katika kika cha leo kamati ya Uongozi wa Baraza umeyajadili kwa kina mapendekezo hayo na kukubaliana kuyawakilisha katika baraza kubwa la Vyama vya Siasa ili kupitisha kwa hatua zaidi za utekelezaji. 

Miongoni mwa mapendekezo yaliyojadiliwa ni pamoja na Vyama vya Siasa kuwa na Sera ya Jinsia na Mfumo mahususi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi wa siasa. 

Kikao hiki cha mashauriano kitaendelea kesho, tarehe 13 Juni 2022 mbapo mapendekezo hayo yatawasilishwa kwa wajumbe wote wa Vyama vya Siasa kupitishwa kwa hatua zaidi.