WASTAAFU WANENA YAMOYONI, ZSSF NI TAASISI YA KUPIGIWA MFANOWastaafu wanapokea pencheni zao kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wamezitaka tasisi nyengine za Serikali na zisizo za Serikali kuiga mfano wa ZSSF katika kuboresha huduma zao na kuondoka usumbufu Kwa wananchi.


Akizungumza mara baada ya kuhakiki taarifa zake Bw. Mohd Juma huko katika ukumbu wa walimu TC Dunga Wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja.

Amesema ZSSF ni tasisi ya kupigiwa mfano kwani wamekuwa akitoa huduma nzuri na zinazokwenda na wakati jambo linaloondoa usumbufu Kwa wateja wake .

" ZSSF wanatutimia ujumbe kwenye simu zetu za mkoni kutukumbusha siku za uhakiki pia tunapokuja kujihakiki hatuchukui ata dakika tatu tushamaliza kusema kweli zoezi linaenda kwa haraka, nichukue fursa hii kuwapongeza kwa hili hakika hii ni taasisi ya kupigiwa mfano "

Aidha ameongeza kwa kuwaomba ZSSF kuongeza kiwango cha  pencheni ili kuwenda sambamba na hali ya kiuchumi.

Kwaupende wake mkuu wa kituo cha uhakiki Mkoa wa Kaskazini na Mkoa wa Kusini Unguja Bw. Omar Nasib Ramadhani ametoa wito Kwa wastaafu kutumia vizuri pencheni zao Ili kujikwamua na hali ngumu ya kimaisha.

Sambamba na hayo amesema ZSSF imepokea maoni ya wastaafu hao na wanaahidi kuyafanyia kazi Kwa haraka zaidi.


Jumla ya wastaafu 400 wanatarajia kuhakikiwa taarifa zao katika kituo cha ukumbi wa walimu TC Dunga Wilaya ya kati Mkoa wa Kasini Unguja.