ZSSF YATARAJIA KUHAKIKI WASTAAFU ELFU KUMI UNGUJANA NA PEMBA


Jumla ya wastaafu elfu kumi na mbili wa mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF wanatarajiwa kuhakikiwa taarifa zao katika mwezi July 2022 ambapo zoezi  limeanza rasmi Leo.

Akizungumza wakati wa zoezi Hilo likiendelea Afisa mafao kutoka ZSSF Bw. Abdalla Mohd amesema lengo la kufanya uhakiki huo ni kuwaondoshea usumbufu wastaafu wakati wa kuchukua pencheni kwa kupata usahihi wa taarifa zao.

Akitoa ufanunuzi juu ya kuwepo Kwa posho ya nauli Kwa wastaafu mkuu wa uhakiki Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja Bw. Omar Nasib Ramadhani amesema Kwasasahivi bado swala hilo halijawekwa katika Mipango ila hali ikiruhusu basi litakuwepo.

Aidha ameongeza Kwa kusema katika Wilaya mbili za Mkoa wa Kaskazini wanatarajia kuhakiki wastaafu 700 ambapo hadi Sasa zoezi linaendelea vizuri.

Akizungumza mara baada ya kuhakiki taarifa zake Bw. Khamis Pandu Subuki   wamewashajihisha wastaafu wenzake kutumia vituo vilivyopo katika mikoa Yao ili kuepuka usumbufu wa kufata huduma hio Mjini.

Zoezi la uhakika Kwa wastaafu wanapokea pencheni katika mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF ambalo hufanyika Kila baada ya miezi 6 limeanza rasmi Leo July 2, 2022 ambapo linatarajiwa kukamilika July 8 2022.