Vyama vya siasa nchini vinatelekeza kwa vitendo azma ya Serikali kuu ya kurashimisha usawa wa kijinsia kwa kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi na uongozi.
Hayo yamesemwa na Mtaalam wa mambo ya sera kutoka TGNP Deogratis Temba wakati wa mafunzo ya kuwawezesha wataalamu wa chama cha CUF kukaa na kuandaa sera ya uwasa wa jinsia huko katika makao makuu ya chama hicho Mtendeni Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.
Amesema baada ya maazimio ya mkutano wa baraza la vyama vya siasa nchini kupitisha sera hio chama hicho kimepokea vizuri pendekezo hilo kwa kuandaa program maalum za kuwawezesha wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi kwanzia ngazi za tawi, kata na hadi kwenye uchaguzi mkuu.
Kwaupande wake Katibu wa kikosi kazi kutoka cha cha wananchi CUF Bw. Ali Juma Khamis amesema katika chama hicho wameadaa fungu maalum kwaajili ya wanawake ili kuwashajihisha wanawake kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi za uongozi.
Aidha ameutaka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuendelea kutoa mafunzo ya kuweka usawa wa kijinsia kwani bado watu wanahitaji kupatiwa elimu hio ili kufikia azma ya 50 kwa 50.
Nae afisa dawatia kutoka chama cha wananchi CUF Bi.Asya Hassan Hamadi amesema sera hio italeta muamko kwa wanawake kujiamini na kujitokeza kwenye uchaguzi mbalimbali.
“wanawake tusiwe waoga tujiamini katika sekta tofauti kwani tunaweza kama alivyoweza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ambae yeye ni mfano mzuri kwa wanawake wote ”
Kwasasa jumla ya vyama 8 vya siasa nchini vimepatiwa mafunzo hayo ya kuwawezesha wanawake katika nafasi za uongozi ambavyo ni CCM, CUF, CUK, ACT WAZALENDO, ADA TADEA , ADC NA AAFBA CHAMA CHA WAKULIMA.