ZSSF YAZIDI KUBORESHA HUDUMA ZAKE SASA YASHUKA KWA MASHEHA



Katika kuadhimisha wiki ya huduma Kwa wateja Dunia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF umetoa madaftari ya taafira za wanachama Kwa masheha wa shehia tofauti za mikoa yote ya Unguja.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko huo Bw. Nassor Shaabani Ameir huko katika ofisi za ZSSF Kilimani mnara wa mbao mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Amesema lengo la kutoa madaftari hayo ni kupata taarifa za wanachama pindipo wanapohama shehia Moja kwenda nyengine au kufariki Dunia, pia kuwapa elimu wananchi wasiojua lengo na dhamira ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kupitia masheha.

"Katika kushirikiana na watendeaji wa serikali za mitaa Ili kusaidia kurahisisha ufanisi wa taarifa za wanachama " Ameaema Bw. Nassor Shaabani Ameir.


Wakizungumza mara baada ya kupokea madaftari hayo wenyeviti wa masheha hao wamesema kupitia utaratibu huo utasaidia kurahisisha kazi kwani masheha wapo karibu zaidi na wananchi pia wameahidi kuyatendea kazi Yale yote walioelekezwa.


Wiki ya huduma Kwa wateja Dunia huadhimishwa Kila wiki ya kwanza ya mwezi  October ya Kila mwaka ambapo Kwa ZSSF wameadhimisha Kwa kutoa huduma tofauti na wanazotoa Kila siku Kwanzia tarehe 3 hadi tarehe 7, sambamba na kutoa madaftari Kwa wenyeviti wa masheha pamoja na kutoa zawadi mbalimbli Kwa wanachama wao waliofika na kupata huduma osifini hapo.