UFARANSA YATUMA KIKOSI KUCHUNGUZA AJALI YA NDEGESerikali ya Ufaransa kupitia ubalozi wake uliopo jijini Dar Es Salaam imetangaza kutuma kikosi cha wataalamu wa masuala ya usalama wa ndege kusaidia uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka Jumapili, Novemba, 9/ 2022 mjini Bukoba na kuua watu 19 na 24 wakiokolewa.

Taarifa ya kutumwa kwa kikosi hicho imetolewa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui ambapo wataalamu hao wamewasili tayari

Ndege hio iliyopata ajali imetengenezwa na kampuni ya ATR ambayo inamilikiwa na makampuni mawili makubwa ambayo ni AIRBUS kutoka Ufaransa na LEONARDO kutoka Italia.

Kampuni ya ATR pia imetuma wataalamu wake nchini Tanzania kusaidia uchunguzi kama inavyotakiwa na sheria za kimataifa za usalama wa anga.

Ndege iliyopata ajali imetengenezwa na kampuni ya ATR ambayo inamilikiwa na makampuni mawili makubwa ambayo ni AIRBUS kutoka Ufaransa na LEONARDO kutoka Italia.

Kampuni ya ATR pia imetuma wataalamu wake nchini Tanzania kusaidia uchunguzi kama inavyotakiwa na sheria za kimataifa za usalama wa anga.