Wananchi wametakiwa kufuata maelekezo wanayopewa na viongozi wa kamati za maafa mara tu inapotokezea tatizo la dharura au majanga .
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Uperesheni na Huduma za Kibinaadamu Haji Faki Hamduni katika ukumbi wa Kukabiliana na Maafa , Maruhubi amesema hivi sasa kumekuwa na matokeo mengi ya majanga ambayo yanatokea katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar hivyo wananchi wanatakiwa kufuata maelekezo ya viongozi hao ili kuepusha maafa .
Alisema Kamisheni ya maafa inautaratibu wa kutoa elimu kupitia kamati za maafa za shehia mbali mbali ili kuwajengea uelewa wa kukabiliana na majanga yakitokea katika maeneo yao pamoja na kuwa mabalozi kwa jamii .
Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Juma Abdalla Hamad amesema kupitia mapendekezo ya kamati ya kukabiliana na maafa ya Wilaya ya Magharibi ‘A’ kutasaidia kuandaa mbinu ya kugawana majukumu ya kiutendaji
Alieleza kuwa Kikao cha kujadili mapendekezo ya mpango kazi wa kukabiliana na maafa kitasaidia kuandaa mbinu bora ya kujihami wakati wa dharura kama upepo, ajali, moto, mripuko wa maradhi na mengineyo .
Amesema mpango huo ni muendelezo kwa watendaji kutoka Taasisi mbali mbali kwa kupanga utaratibu wa kila mdau kutekeleza majukumu yake wakati wa dharura ,majanga au maafa .
Kwa Upande wa Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi Bandarini, ASF . Jokha Patrick Bundala amesema katika utekelezaji wa majukumu ya zimamoto ni kuzimamoto, kuokoa waganga na kuwaelimisha jamii kupitia vyombo vya habari.
Akitoa wito kwa jamii aliwataka kutoa taarifa mapema katika vituo vya zimamoto na uokozi kwa namba 114 ili katua za haraka ziweze kuchukuliwa.