ZSSF YATEKELEZA KWA VITENDO AZMA YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBARWatendeaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wametakiwa kupanua wigo na kuendelea kuwa wabunifu Ili kuhakikisha wanachama nawapata stahiki zao Kwa mujibu wa sheria na kuwajengea uwezo wasio wanachama kujiunga na mfuko huo.


Ameyasema hayo Katibu mkuu Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Bw. Islam Seif Salum wakati wa mafunzo Kwa wastaafu watarajiwa huko katika ukumbi wa Michenzani Mall Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.


Amesema ZSSF inawajibu wa kuhakikisha inawapa mafunzo wastaafu wao Ili wajue jinsigani wanatumia mafao Yao hadi  wanafikia malengo waliojiwekea.

Aidha ameipongeza ZSSF Kwa kutekeleza Kwa vitendo ilani ya chama Cha Mapinduzi na ahadi za Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi ya kutoa huduma bora Kwa wananchi.


Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Bw. Nassor Shaabani Ameir amesema wanaendelea kufanya uhakiki Kwa wanachama wote wa Serikali na sekta binafsi ili kupata usawa wa taarifa za uhakika pamoja  jambo ambalo litasaidia kupata fedha zao Kwa wakati mara baada ya kustaafu.


Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Bw Mussa Ame Mussa amesema mafunzo hayo yamewasaidia kujua  vipi wataendesha maisha yao mara baada ya kustaafu pia amewaomba ZSSF kuanda magroup ya mitandao ya kijimii katika kutoa mafunzo.


Mafunzo hayo ya siku Moja yenye lengo la kuweza na kuwasaidia wastaafu watarajiwa kufikia malengo waliokusudia katika kuendeleza maisha yao mara baada ya kustaafu ambapo Kwa mwaka 2022 jumla ya wanachana150 wanatarajiwa kustaafu.