ZSSF YAZINDUA FAO JIPYA LA UPOTEVU WA AJIRA



Katika kuimarisha huduma na kulipa mafao bora Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wamezindua rasmin FAO LA UPOTEVU WA AJIRA ambalo litamuwezesha mwanachama kupata fedha taslim kulingana na vigezo vilivyowekwa kisheria mara baada ya kupoteza ajira yake.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo sambamba na mkutano wa saba wa wadau wa ZSSF Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Riziki Pembe Juma huko kwenye ukumbi wa Michenzani Mall Mjini Zanzibar.

Amesema mafao hayo mapya yatakwenda kukomboa vijana wengi ambao kazi zao ni zamikataba mifupi ( ajira sizizo rasmin ) ambapo mara nyingi wanapopoteza ajira zao wanakosa kipato cha kukizi maisha.

Aidha Mh. Riziki amewataka wajiri kutofanya udanganyifu wakati wa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao Kwavile sasa wamepatiwa fursa ya kutuma michango hio popote walipo.

Kwa upande wake mwenye kiti wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko huo Dk. Huda Ahmed Yussuf amesema ZSSF tayari inakaribia robo Karne ikiwa inatoa mafao Kwa wanachama Kwa wakati unaostahiki pamoja na kuimarisha mafao.

Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Bw. Nassor Shaabani Ameir amewataka wanachama kuwa mstari wa mbele katika kuchukua nyumba za gharama nafuu Ili wapate kunufaika na miradi inayowekezwa.


Mkutano wa sita wa wadau wa ZSSF umeenda sambamba na utoaji wa tunzo Kwa tasisi, mashirika na wanachama wanaochangia vizuri ambapo Wizara ya maji, nishati na madini, Idara ya Uvuvi ( ZAFICO), International school of Zanzibar, Boat boys wamepokea tunzo hizo na kwaupande wa Mfuko wa hiyari ni Bi. Aisha Zahour Kombo na Bi.Sakina Hamid Hafidh  wamepokea tunzo hizo.