ZSSF: SWALA LA BIMA YA AFYA LIMEFIKIA ASILIMIA 90

 


Mfuko wa Hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF umesema swala la bima ya afya kwa wanachama na wastaafu wake limefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake ambapo Serikali kuu inalifanyia kazi.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi la uhakiki likiendelea huko katika Ofisi za ZSSF Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja Kaimu mkuu kitengo cha uhusiano na masoko Bi. Raya Hamdani amesema swala la bima ya afya linafanyika kwa kushirikiana na tasisi tofauti ikiwemo Shirika la bim, Wira ya Afya na Wizara ya Fedha ili kuwapatia wananchi huduma hio.


Aidha Biraya amesema zoezi la uhakiki linaendeleakufanyika hadi harehe 8 Januari ambapo katika kituo hicho tayari wanachama Zaidi ya 400 wameshahakikiwa taarifa zao.


Kwaupande wake Mkuu wa kituo cha uhakiki Mkoa wa Kusini na Kaskazini Bw.Omar Nasib Ramadhan amesema katika kituo hicho wanatarajia kuhakiki jumla wa wastaafu 600 ambapo zoezi hilo linaendelea vizuri licha ya changamoto ndogondogo zinazojitokeza.