ZSSF YAFANYA UHAKIKI WA WASTAAFU

 Zoezi la uhakika Kwa wastaafu wanaopokea pencheni zao kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF limeanza rasmin leo January 2/ 2023 ambapo jumla ya wastaafu kumi na tatu elfu wanatarajiwa kuhakikiwa taarifa zao.


Akizungumza na waandishi wa habari huko katika viwanja vya kufurahishia watoto Kariakoo Kaimu mkuu kitengo Cha uhusiano na masoko ZSSF Bi Raya Hamdani Khamis amesema uhakiki huo utaendelea hadi tarehe 8 /2023 katika vituo vyote vya Unguja na Pemba .


Aidha amesema zoezi hilo inawawezesha kujua idadi ya wastaafu waliongezeka na kupungu ndani ya kipindi cha miezi 6 na kujipanga vizuri katika kuondoa usumbufu wa kuchelewa kwa pencheni au kuzuiwa .


Akitolea ufafanuzi swala la kuongezewa kwa pencheni wastaafu Bi. Raya amesema swala hili wanalifanyia kazi na wanalitizama Kwa jicho la huruma haswa waakati huu wa mfumoko wa bei.


Kwaupande wake mkuu wa vituo vya uhakika Mkoa wa Kaskazini na Kusini Bw. Omar Nasib Ramadhan amesema katika Mkoa wa Kaskazini wanatajia kuhakiki wastaafu wasiopungua 1000 ambapo wazee wamejitikeza kwawingi na kuhakikiwa.


Akitoa shukran zake mstaafu kutoka Wizara ya Elimu Bi. Fatma Juma ameishukuru ZSSF Kwa kuhakikisha kila linapofika zoezi hili wanajipanga vizuri na kutoa huduma kwa wakati .

Sambamba na hayo Bi. Fatma ameziomba tasisi nyengine kuiga mfano wa ZSSF ili kurahisisha huduma bora kwa wananchi.

Zoezi la uhakika Kwa wastaafu wa ZSSF hufanyika Kila baada ya miezi sita kila mwaka kwa lengo la kuwatambua wastaafu wake na kuweza kujipanga vyema katika bajet zake.